Friday, August 9, 2013

"SIHITAJI MUME, ***MUME WANGU NI KAZI", :**SALAMA JABU(NISHA).MREMBO anayekuja juu katika uaandaaji wa filamu Bongo Salma Jabu ‘Nisha’ ametoa mpya pale alipotangaza kuwa hana mahusiano na mwanaume yoyote na kuonyesha pete yake aliyodai ndio mumewe akiongea na mwandishi aliyetaka kujua kuhusu maisha yake ya mahusiano na kumtaka msanii atumie fursa hiyo kumtambulisha mpenzi huyo ambaye anaye na kusema hana mwanaume.

Unaiona pete hii kwa wengine ni ishara ya pingu au ndoa na mimi pete hii inasimama kama alama ya mume wangu lakini mume wangu mimi ni kazi yangu ya filamu na si kingine naipenda sana kazi yangu na kuona au kuhisi pengine kama nikiwa na mume anaweza kunizuia nisifanye kazi ambayo ndio hobby yangu,anadai Nisha.

Nisha ni mwigizaji ambaye amekuwa akifanya vizuri katika utayarishaji wa filamu za vichekesho huku mara nyingi akimshirikisha mchekesha mkongwe nchini King Majuto Komedi alizoandaa Nisha na kutikisa ni Pusi na Paku, Tikisa na filamu ya Macho yangu, pia siku za nyuma iliwahi kuripotiwa kuwa msanii huyo kuwa na mahusiano msanii wa hip hop Ney wa Mitego kitu anachokipinga Nisha.


insurance,loans, n.k

TOA MAONI YAKO HAPA